Mama Kanumba, Lulu watumiwa ujumbe mzito

Muigizaji Mkongwe wa filamu nchini, Natasha Mamvi amefunguka na kutoa pole kwa Wazazi wa wasanii, Kanumba na Lulu baada ya Mahakama Kuu kutoa hukumu kwa muigizaji lulu kutokana na kukutwa na kosa la kuua bila kukusudia kwa Muigizaji Kanumba

Bi Natasha ametumia ukurasa wake wa Instagram leo na kuwaomba wazazi hao baada ya mahakama kutoa tamko lake siku ya jana sasa wazazi hao wanapaswa kumshukuru Mungu kwa yaliyotokea na kisha wasamehane ila kutimiza agizo la msamaha.
"Ninachukua nafasi hii kuwapa pole wanawake wenzangu mama lulu na mama kanumba kwa vile wote mmepatwa na uchungu sawa. Mama Lulu ni kama umekatwa mkono wa kuume lakini iko siku soon mwanao atarejea mikononi mwako tena na maisha yataendelea, Lakini  kwa upande wa Flora mwanae ndio hatarudi tena katika hili hakuna wa kusema ana uchungu wa afadhali uchungu wa mtoto ni uleule tu asipokuwepo mikononi mwako" - Natasha
Ameongeza "Swala ni mzidi kuomba faraja kwa Mungu ili ndani yenu muwe na roho ya msamaha msameheane ili mtimize lile agizo la kusamehe zaidi ya mara 70! watoto wamewapitisha katika machungu haya mnayoyapitia na wala sio swala la kuwalaumu ila mzidi kuwaombea" 
Bi Natasha amesema juzi alikutana na Lulu na akawa ameongea naye kuhusiana na kitu kilichopo mbele yake na kwamba alimuandaa kimawazo huku akimkumbusha kwamba anapaswa kuamini katika muujiza.
"Hata hivyo Mkongwe huyo wa filamu amemgeukia Mama Kanumba na kumkumbusha kwamba "Flora (mama Kanumba) jana ulienda kaburini na kulia machozi ya uchungu uliponyanyuka pale naomba uwe umenyanyuka Flora mpya yaache maumivu na machungu pale kaburini. Najua hautasahau kamwe uchungu wa kuondokewa na mtoto lakinimwombe Mungu akupe nguvu ya kuendelea mbele". Natasha


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo