Rais Magufuli ameeleza hayo leo Oktoba 3, 2017 wakati akihotubia kwenye Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (Alat) ambao umefanyika Dar es Salaam na kusema kuwa kiongozi huyo ni mfano mzuri kwa viongozi wengi kutokana na uchapaji wake kazi.
"Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alipojaribu kuzungumza kidogo kuhusu madawa ya kulevya vita ikawa kubwa kweli kwake, hajasoma hajafanya nini mimi kwangu hata hajui 'A' ilimradi anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri, kwani Wenyeviti mliopo hapa wote mmesoma? Kwani Halmshauri haziendi vizuri? Kuna wasomi wengine wametuangusha kinachohitajika ni uzalendo na kuipenda Tanzania na huo ndiyo moyo tunaotaka kuujenga kwa Watanzania kuipenda Tanzania" alisema Magufuli
Miezi kadhaa iliyopita Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, aliamua kufungua shauri mbele ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ili mamlaka hiyo ishughulikie suala la utata wa vyeti na jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kadri Sheria za nchi zinavyotaka ili kumaliza utata uliopo juu ya jambo hilo, jambo ambalo bado linaendelea katika hatua mbalimbali.
