Askofu amesema kwamba dunia inabadilika kwa kasi na Tanzania ipo nyuma hivyo amesisistiza elimu izingatiwe ili kuweza kufukuzia maendeleo ya nchi zilizoendelea angalau kuwafikia mataifa ya Magharibi Kiuchumi.
Mbali na hayo Wakuu wa shule nchini wametakiwa kusimamia shule vizuri ili kuimarisha elimu na kutoa wataalamu wenye elimu bora hasa kipindi hiki serikali ikiwa na sera ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda na wataalamu wakihitajika kwa wingi.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Lupembe Njombe, Jorum Hongoli nakuwafikia moja kwa moja wakuu wa shule za kikatoliki za msingi na sekondali jimbo la katoliki Njombe ambao wanakutanishwa katika kongamano la Elimu la katoliki mkoa wa Njombe.
"Unapokuwa umekabidhiwa dhamana ni lazima ufanye kitu cha tofauti. Kwanza shule yako inaonekane ni ya tofauti na hata kama ni Sekondari basi ionekane na utofauti, Kuonyesha utofauti naousema ni kwamba shule ifanye vizuri ili hata shule zingine waje kujifunza kutoka kwako" alisema Mhe. Hongoli.
