Afisa wanyamapori asimishwa kazi kwa Kumchoma Moto Mwananchi

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Mahenge amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani humo, kumsimamisha kazi afisa wanyamapori wa wilaya hiyo, Bw. Ernest Nombo kwa tuhuma za kuhusika kumchoma moto mwanachi mmoja mkazi wa kijiji cha mtanda akimtuhumu kuvamia hifadhi ya wanyamapori namtanda na kulima zao la mpunga.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Mahenge ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata ya Lusewa, wakilalamikia vitendo vya unyanyasaji vilivyofanywa na afisa wanyamapori huyo kwa kumchoma moto mwananchi wa kijiji cha Mtanda,Bw. Amosi Kifaru kwa kumtandikia nyasi chini, kumlaza na kisha kuwasha moto akimtuhumu kuvamia hifadhi ya wanyampori ya mtanda na kulima mpunga.

Malalamiko hayo ya wananchi wa Lusewa-Namtumbo yakamlazimu mkuu huyo wa mkoa kutoa maagizo kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Namtumbo, kumsimamisha kazi mara moja afisa wanyamapori huyo, Bw.Ernes Nombo kwa hatua zaidi.

Kutokana na kadhia hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amesema itaundwa tume maalumu kuchunguza vitendo hivyo ili kuwabaini watumishi wengine waliohusika katika vitendo hivyo vya unyanyasaji ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo