Maafa yaikumba wilaya ya Muleba Kagera, Nyumba zaezuliwa, Angalia hapa

Wilaya ya Muleba iliyopo mkoani Kagera, imekumbwa na maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa ya upepo na mawe, iliyonyesha jana Jumanne, saa saba mchana na kusababisha athari katika kata tatu.

Maeneo yaliyoathirika ni kama yanavyoonekana katika mabano: Kata ya Mubunda, (nyumba moja), (mazao ya mihogo) na (migomba), kata ya Buganguzi (nyumba 18) na chumba kimoja cha darasa la sekondari ya Rukindo, kimeezuliwa.

Eneo jingine ni kata ya Ibuga ambapo nyumba, shule ya msingi Ruzinga, chumba kimoja cha darasa kimeezuliwa, pamoja na choo na jiko.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa Azam TV, Junior Mwemezi, aliyepo mkoani Kagera, wanafunzi wawili wamejeruhiwa na kupelekwa kituo cha afya cha Kamachumu (Kabanga).

 Taarifa hizo ni za awali tu, kwani tathmini halisi bado inaendelea kufanyika katika maeneo hayo yaliyoathirika









JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo