Taarifa zilizotufikia hivi sasa ni kwamba Mtangazaji wa EFM Denis Rupia maarufu kama Chogo amefariki dunia
Taarifa hizi zimetolewa na Meneja Mkuu wa EFM Denis Sebo jukwaani usiku huu wakati wa Tamasha la Muziki Mnene linalofanyika Mubashara jijini DSM
Hali hiyo imepelekea matangazo hayo ya moja kwa moja kukatishwa
Hii hapa chini ndiyo taarifa ya awali iliyotolewa na EFM
"Uongozi na Wafanyakazi wa E-FM,TV-E kwa majonzi na masikitiko makubwa tunatangaza kuondokewa na Mwanafamilia Mwenzetu Dennis Rupia (Chogo),aliyefarika Dunia baada ya kuugua kwa kipindi cha muda mfupi.
Aidha kwa taarifa zaidi tataendelea kufahamishana taratibu za kumpumzisha mpendwa wetu kupitia vyanzo mbalimbali vya mawasiliano.
Hakika ni kipindi Kigumu kwetu,Wasikilizaji wa Redio na familia kwa ujumla tuendelee kuombea Mpendwa wetu" ,E-FM.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN
