skip to main |
skip to sidebar
Team CUF Lipumba yakataliwa na jaji leo
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake wamekwama mahakamani leo baada ya Jaji Ndyansobera kukataa maombi ya Profesa Lipumba na kundi lake.
Jaji Ndyansobera amekataa kufuta kesi Namba 28/2017 kama ilivyoombwa na Lipumba ili wapate Ruzuku ya Chama Cha Wananchi wa CUF inayofikia shilingi billion moja na million mia nne toka Julai mwaka jana.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande amefunguka na kusema kufuatia maamuzi haya ya mahakama hivyo hakuna pesa ambayo Profesa Lipumba anaweza kuchukua hata shilingi moja.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi