Kamanda Cameron Steily akimueleza jambo Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipomtembelea ofisini kwake leo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam kulia akiwa na Kamanda Cameron Steily ofisini kwake leo .
Kamanda Cameron Steily kushoto akimkabidhi Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita zawadi , alipomtembelea ofisini kwake leo kwa lengo la kusalimia.MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ametembelewa ofisini kwake na Kamanda wa kikosi cha Maji Nchini Australia Cameron Steily ambapo pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kumkaribisha jijini hapa. Kamanda Cameron ataondoka jijini hapa Mei 15.
