Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma akihotubia katika moja ya mkutano wake kipindi cha kampeni za Uchaguzi 2015.
Msukuma amedai kuwa wabunge hao baada ya kupita katika chaguzi zao wamekuwa wakiwasahau waganga hao wa kienyeji na kufikia hatua ya kuwatumia polisi ili wawakamate badala ya kuwasaidia, hivyo Mbunge huyo ameiomba serikali japo kuwajengea hata chuo tu waganga hao wa kienyeji kwa kuwa wamekuwa wakifanya mambo mengi yanayosaidia katika jamii.
"Nimekuwa nikisikia wabunge wakiwatetea sana wasanii humu ndani wanawasahau waganga wa kienyeji. Kwa karama niliyonayo nikiwaangalia Wabunge humu ndani wakati wa uchaguzi wote hakuna ambaye hakupita kwa waganga wa kienyeji, labda wawili ambao hawakupita kwa waganga akiwepo Mh. Joseph Selasini lakini Mh. Spika siyo wabunge tu pekee yao hata jamii nzima, lakini cha ajabu waganga hawa baada ya Uchaguzi tunawatelekeza na kuwaitia polisi" alisema Msukuma