Kijana wa miaka 22 afariki dunia baada ya kuzama mtoni

Kijana mmoja  anaetambulika kwa Jina la Suleiman Mtumwa Suleiman mwenye umri wa miaka 22 amefariki dunia  baada ya kuzama katika Mto wa Faki Abuu  hapo  jana huko kilombero  Wilaya ya kaskazini B.

Wakizungumza na mwanahabari wetu baadhi ya mashuhuda katika tukio hilo Hija Ali Hija na Habiba Mohamed wamesema tukio hilo limetoka jana majira ya saa 11 jioni na jitihada za uwokozi zilifanyika lakini alishindikana kupatikana hadi leo baada ya kikosi cha uwokozi kufika katika tukio hilo.
 Kwaupande wake Daktari wazamu wa Hospitali ya Kivunge Makame Mdungi Makame amethibitisha kupokea mwili wa kijana huyo aliyefariki dunia  baada ya kuzama  katika mto, huko kilombero na amesema kifo chake kimesababishwa na kunywa maji mengi  katika mto huo.
Aidha Daktari huyo alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari  kwa  kuwadhibiti watoto wao kucheza  karibu na mito na maeneo yaliyotuama maji ili kuepukana  na majanga yanayoweza kujitokeza.
Matukio ya kuzama kwa watoto katika kijiji cha kilombero hutokea mara kwa mara hususani kipindi kama hichi cha mvua.

Na:Amina Omar Zanzibar24.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo