Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akiwa ndani ya basi la Mwendokasi pamoja na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (anayetazama kadi yake ya DART) wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim wakati wakiwa ndani ya moja ya basi la DART wakati wakitokea kituo kikuu cha BRT-Kivukoni kuelekea Ubungo kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipanda basi la DART-Maarufu kama Mabasi ya Mwendokasi katika eneo la Kivukoni wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ndani ya basi la Mwendokasi wakati akielekea Ubungo kuhudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za juu Ubungo interchange, Ubungo jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU



