Angalia Picha "Mtoboa Macho" akifikishwa Mahakamani hii leo

Mkazi wa buguruni kwa mnyamani anayetuhumiwa kuwachoma watu visu na kisha kuwatoboa macho, Salum Henjewele maarufu kama Scorpion amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Ilala na kusomewa tena shtaka la unyang’anyi  wa kutumia silaha .
Scorpion ambaye alikamatwa baada ya kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Ally mkazi wa mabibo Hostel, alipandishwa kizimbania mahakamani hapo kwa mara ya kwanza September 23 mwaka huu.
Kesi hiyo inayosikilizwa na hakimu Adolf Sachore leo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Source: Mwananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo