Mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24) amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini hapa baada ya kung’atwa theluthi tatu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi.
Tukio hilo la aina yake, lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa kumkia Sikukuu ya Idd el Hajj. Mamba ambaye hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi.
Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake.
“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema.
Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande.
chanzo:mwananchi
chanzo:mwananchi
