Matukio ya ukatili wilayani Makete mkoani Njombe yameendelea kutokea ambapo katika kitongoji cha Mang'oto kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo wilayani hapa mwili wa mtoto wa kiume aliyetajwa kwa la John Kyando (2) umekutwa umetupwa mtoni ukiwa umeharibika vibaya
Kwa mujibu wa mama Mzazi wa marehemu Bi. Vumilia Kyando (17) mkazi wa Bulongwa wilayani hapa ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji hayo amesema tukio hilo limefanyika wiki tatu zilizopita huku yeye akishuhudia na tukio la kuonekana mwili wa marehemu ukiwa majini limetokea Jumamosi Julai 16 mwaka huu majira ya asubuhi
Amesema alimpata mwanaume aliyemtaja kwa jina moja la Bahati ambaye walianzisha uhusiano wa kimapenzi wakati yeye akifanya kazi ya baa kwenye baa mpya iliyoanzishwa kijijini hapo, ambapo ilionekana kama mtoto huyo anawatinga katika mahusiano yao na ndipo mwanaume huyo alipomshawishi wamuue na yeye akakubali kushiriki mauaji hayo

Bi. Kyando amesema siku ya tukio alipigiwa simu na mumewe huyo waongozane kwenda mtoni kutekeleza mauaji hayo, na kwa maelezo yake amesema walipofika eneo la tukio mpenzi wake alimchukua mtoto na kumfanyia mauaji huku akimwambia mwanamke huyo ambaye ni mama mzazi wa mtoto aangalie watu kama wanapita eneo hilo wasije kuwaona
"Mimi nilikuwa nimemvalisha mwanagu nguo lakini yeye alimvua ndipo akatekeleza mauaji hayo huku mimi nikiwa kwa juu kule naangalia watu kama alivyoniagiza" amesema Vumi
Ameongeza kuwa mpenzi wake huyo alimwambia endapo ataulizwa na mtu yeyote kuhusu kitendo hicho asiseme na akiulizwa alipo mtoto aseme amempeleka kwa bibi yake jambo ambalo alilitekeleza

Hata hiyo katika maelezo yake na mwandishi wetu hakueleza mtoto huyo aliuawaje ingawa kwa taarifa za awali zinaonesha mtoto huyo aliuawa kwa kunyongwa shingo mpaka kufa na kisha kutupwa kwenye mto wenye maji
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Maria Mahenge amesema tukio hilo si tu linahuzunisha lakini limechafua taswira nzima ya kijiji chao, na hasa ukizingatia tukio hilo linadaiwa kufanywa na mama wa marehemu ambaye si mzaliwa wa kijiji hicho na badala yake alifika hapo kikazi tu
Amesema baada ya watu kutomuona mtuhumiwa huyo na mtoto wake kama mwanzoni walilazimika kumuuliza na aliwajibu kuwa amempeleka kwa bibi yake na anatunzwa huko
Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Huruma Mbilinyi amesema tukio hilo linahuzunisha na kuwaomba wananchi wa kijiji hicho kushirikiana pamoja na viongozi wao kupata taarifa sahihi za wageni wanaofika kijijini hapo kufanya kazi ili iwe rahisi kufuatilia mienendo yao tangu walikotoka
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Happyniko Michael Sanga amekiri kuwepo kwa tukio hilo katika kijiji chake na kusema kwamba baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji za tukio hilo, walilazimika kumbana binti huyo ambaye toka awali hawakuridhishwa sana na majibu yake kuwa amempeleka kwa bibi yake, na ndipo walipombana na kukiri kuwa ameuawa na kuwapeleka hadi eneo la tukio ulipokutwa mwili huo
Amesema Hali hiyo iliwalazimu kutoa taarifa kituo cha polisi Makete ambapo jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umeharibika vibaya baada ya kukaa kwenye maji kwa muda wa wiki 3, na baada ya kuchukua taarifa zao walishauriana kwa pamoja na uongozi wa kijiji na kata kuuzika mwili wa marehemu jirani na eneo la tukio kutokana na uharibifu wa mwili huo
Amesema baada ya kuuzika mwili wa marehemu polisi walifika kijijini hapo kufanya mahojiano na baadhi ya watu wakiwemo viongozi na pia kumchukua mtuhumiwa ambaye ni mama mzazi wa marehemu kumpeleka kituo cha polisi Makete kwa hatua zaidi za kisheria
Taarifa za tukio hilo zimetolewa na watoto waliokuwa wakichunga ng'ombe jirani na mto huo ambapo wakati wakienda kuwanywesha maji ng'ombe hao mtoni majira ya jioni kabla ya kuwarudisha nyumbani ndipo walipuona mwili wa marehemu na kupeleka taarifa za tukio hilo kijijini hapo

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Pudensiana Protas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwa maelezo yake amesema mtuhumiwa huyo amekiri kutenda tukio hilo lakini kamanda hakusema kama alishirikiana na mtu kutekelezaq mauaji hayo na kutoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia uamuzi wa kukatisha uhai wa binadamu yeyote kwani ni kinyume cha sheria, na upelelezi ukikamilika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani