Mbunge wa Kigoma Mjini
(ACT-WAZALENDO), Zitto Kabwe (kulia) akitoka katika kituo kikuu cha
polisi jijini Dar es Salaam baada ya mahojiano.
MBUNGE wa Kigoma Mjini ambaye
pia ni Kiongozi Mkuu chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, mapema leo
aliitikia wito kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam,Camilius Wambura, wa kufika katika kituo kikuu cha polisi polisi
jijini Dar alipohojiwa kwa zaidi ya saa tatu.
Akizungumza na wanahabari kituoni hapo
mara baada ya kutoka, mwanasheria wake, Stephan Mwakibola, alisema kuwa
kiongozi huyo amehojiwa kuhusiana na maudhui ya hotuba ambayo aliitoa
Jumapili iliyopita katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya
Mbagala- Zakhem jijini Dar.
Naye Zitto alisema kuwa anasikitika kuona siku hizi kiongozi wa chama cha siasa anapokwenda kwenye mikutano analazimika afikirie kutafuta maneno ya kuzungumza.
Mwakibola alieleza kuwa polisi
wamemruhusu Zitto kuendelea na shughuli zake za kila siku baada ya
kupewa dhamana, na Jumatano ijayo ametakiwa kuripoti tena polisi. Hata
hivyo, wakili huyo hakuwa tayari kuweka bayana sehemu ya hotuba ambayo
ililileta utata kwa sababu suala hilo bado liko chini ya upelelezi.
NA DENIS MTIMA/GPL