Angalia Ugeni watua Iringa

update 4/4/16 Tumetembelewa na kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Umwagiliaji, Uvuvi, mifugo na Maji chini ya Makamu Mwenyekiti Mh Christine Ishengoma (MB) wakiambatana na Naibu waziri wa kilimo na mifugo Mh William OleNasha (MB) na Naibu waziri wa Maji na umwagiliaji Eng Isack Kapwelwe(MB). Kamati ilitembelea miradi mbali mbali pamoja na Bodi ya nafaka mchanganyiko.Kamati ilitembeea kinu cha Bodi ya nafaka Mchanganyiko na kujionea jinsi kazi inavyo endelea. Kinu hiki ni moja kati ya vinu bodi inavyo miliki ambapo awali vilikuwa chini ya NMC. Changamoto kubwa ni kinu cha Arusha ambapo mpangaji bado hajarejesha kwa serikali juhudi za kurejesha zinaendelea ili bodi hii iwe na uwezo wa kusaga tani 100,000 kwa siku.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo