Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa taarifa kufuatia kuwepo kwa tangazo katika mitandao ya kijamii kuwa kuna ajira zimetolewa katika kada za afya.
Katika taarifa ambayo imetolewa na msemaji wa wizara, Nsachris Mwamwaja imeeleza kuwa tangazo hilo sio sahihi na halina ukweli hivyo wananchi wasilifuate.
“Kuna tangazo kuwa kuna nafasi za kazi katika kada ya afya ambazo ni madaktari, madaktari wa meno, matabibu wasaidizi na wataalamu wa maabara, taarifa hizi sio sahihi,” amesema Mwamwaja.
Aidha msemaji huyo wa wizara amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kutoa taarifa zisizo sahihi kupitia mitandao kwani sinasababisha usumbufu kutoka kwa watu wanaohitaji nafasi hizo, na badala yake wazitumie kwa matumizi yanayofaa.
