Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), leo imewaburuza kwenye Mahakama ya Kisutu jijini Dar, wabunge wa 3 wa Kamati za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotuhumiwa kuomba rushwa kiasi cha Tsh. milioni 30 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro.
Wabunge hao ni Mbunge wa jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola, Mbunge wa Mvomero Mh. Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa Mh.Victor Mwambalaswa.
Taarifa zaidi za tukio hilo zitawajia kadri tutakavyozipata.
