Kamanda Simon Sirro atoa onyo kwa wanasiasa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewataka wanasiasa wanaosababisha kutokea vurugu kutambua kuwa Polisi wapo na watawachukulia hatua wote wanaohusika kusababisha vurugu ambazo zinaweza kusabisha upotevu wa amani nchini.
Kamanda Sirro aliyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa baadhi ya wanachama wa moja ya chama cha siasa katika uchaguzi wa meya wa jiji la Dar es Salaam uliofanyika jana jumamosi.
Alisema hakuna mwanasiasa aliye juu ya sheria na wao kama Jeshi la Polisi watahakikisha wanawachukulia hatua wote wanaohusika kwani watakuwa wanavunja sheria ya nchi.
“Wambie tutawashughulikia kweli kweli … wanafanya vitendo hivyo sababu kuna amani na kama hakuna amani hakuna siasa na kama kuna mwanasiasa anasababisha vurugu huyo sio mwanasiasa,” alisema Kamanda Sirro.
Kamanda alieleza wazi kuwa askari aliowapeleka katika uachaguzi huo ni wachache na siku nyingine ataweka askari wengi zaidi ili kuwazuia wote ambao wanasababisha vurugu na tayari wamefungua jarada kwa ajili ya walio husika na kusababisha vurugu.
Pia Kamanda alizungumzia kitendo cha waandishi wa habari kuzuiliwa kuingia ndani ya chumba cha uchaguzi wakati uchaguzi huo ukiendelea na kuwataka kuwa wavumilivu katika kipindi kama hicho na sababu ya kufanya hivyo ni kuweka usalama kwanza ili kuzuia vitendo vya vurugu.

DSC_0578Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CHADEMA, Halima Mdee akielekea katika gari baada kufika Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya kuwatoa wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wamekamatwa na Polisi kwa madai ya kusababisha vurugu katika Uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu.
DSC_0579Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Chadema, Halima Mdee akiingia katika gari baada kufika Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya kuwatoa wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wamekamatwa na Polisi kwa madai ya kusababisha vurugu katika Uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam.
DSC_0587Baadhi ya wanachama wa CHADEMA wakionyesha ishara ya Mabadiliko baada kufika Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya kuwatoa wanachama wenzao.
DSC_0588Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu akitoka Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya kuwatoa wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa wamekamatwa na Polisi kwa madai ya kusababisha vurugu katika Uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam.
DSC_0591Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu akiondoka Makao Makuu ya Polisi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo