Duu Hii katika katika Umeme Makete kumbe inasababishwa na huyu hapa?

Wilaya ya Makete kwa takribani wiki moja sasa imekuwa kama utaratibu kwa umeme kukatika kwa zaidi ya saa nne na kuendelea huku watumiaji wa umeme wakishindwa kuelewa hatima ya tatizo hilo.

Mwandishi wetu Asukile Mwalwembe amezungukia maeneo mbalimbali ya watumiaji wa umeme wa gridi ya taifa wilayani Makete mkoani Njombe ili kujua hali ilivyo hasa kwa watumiaji wa umeme huo ikiwemo wenye biashara za saloon.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao pamoja na wafanyabiashara wa kata ya Tandala wilayani hapa wamesema wanakaa bila kazi nakupoteza wateja wao hivyo kukosa mapato ya siku pindi umeme unapokatika.

Aidha wananchi hao wameomba shirika la Ugavi wa umeme  Tanzania TANESCO Wilayani Makete kutoa taarifa pindi umeme unapokatika ili kuepuka athari zinaweza kutokea wakati wa kurudisha umeme ikiwemo kuungua kwa vyombo vyao vinavyotumia umeme.

Kwa upande wake meneja wa Shirika La ugavi wa Umeme Tanesco wilaya ya Makete Bw, Ramadhan Mwanga amesema radi pamoja na wananchi kurusha fimbo kwenye nguzo/nyaya za umeme ndicho chanzo cha kukatika kwa umeme na kusema kwamba wanatarajia kuanza kutoa elimu ya matumizi ya umeme hasa kwenye sehemu zilizopitiwa na  mradi wa umeme vijijini REA ili kuepusha changamoto hizo zinazosababisha umeme kukatika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo