Rais Magufuli awataka wapinzania wakubali yaishe

Rais wa awamu ya Tano Dokta John Pombe Magufuli amevitaka vyama vya upinzani nchini kuondoa tofauti zao na badala yake washirikiane pamoja katika kuwatumikia watanzania ili kufanikisha azma ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kuapishwa rasmi na kuwa rais wa Jamhri ya muungano wa Tanzania awamu ya tano Katika Sherehe zilizofanyika JIjini Dar es Salaam.
Kushushwa kwa  Bendela ya Rais inaonesha kufikia ukomo kwa uongozi wa Serikali ya awamu ya nne na sasa imeingia serikali Mpya mbayo ni ya awamu ya tano.
Katika siku hiy ya kuapishwa Dkta Mgufuli mvua ilinyeshapo jambo lililo tafsiriwa kuwa ni kuashiria neema kwani wakulima hutegemea mvua kwa ajili ya kuotesha mazao yao, wafugaji nao hutegemea mvua wakitaraji kustawi kwa malisho ya mifugo yao, na kwa Dokta Magufuli hii ni ishara njema ya kuwatumikia Watanzania.
Hatimae shughuli iliyokuwa Ikisubiriwa na umati wa Watanzania ikawadia, ni rais Mteule kula kiapo cha kuwatumika Watanzania ikimaanisha kupewa mamlaka kamili ya kuiongoza Tanzania kwa nafasi ya Urais.
Asili ya mtanzania kwa kiongozi huyu haikuachwa nyuma ambapo aliweza kukabidhiwa Mkuki pamoja na ngao
Katika Sherehe hiyo viongozi wa Dini nao hawakuwa nyuma katika kuiombea serikali ya awamu ya tano ili kufikia malengo yake kwa kipindi cha miaka 5 ijayo
Rais Magufuli anapata fursa ya kuzungumza na watanzania shabaha yake kuu ni kuwataka wapinzani kushirikiana na Serikali ili kuendelea na ujenzi wa Taifa.
Sherehe Hizo zilizofana zimehudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali ikiwemo umoja wa nchi za afrika mashariki na Afrika kwa ujumla ukiongozwa na Marais, Robert Mughabe wa Zimbabwe, Joseph Kabila wa Demokrasia ya Kongo, Paul Kagame wa Rwanda , Yoeri Museven wa Uganda , Uhuru Kinyatta wa Kenya ,
Wengine ni Edgar Lungu wa Zambia , Filipe Nyusi wa Msumbiji pamoja Jacob Zuma wa Afrika ya kusini.
Hata hivyo zaidi ya mataifa 47 ya nje yametuma wawakilishi wake katika sherehe hizo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo