Nyumba ya msanii Batuli yateketea kwa moto

Nyumba ya muigizaji wa filamu, Batuli imetekea kwa moto.

Nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

“Nilikuwa saluni najiandaa ili niende kwenye fainali za TMT ndipo nilipopigiwa simu na majirani majira ya saa tatu usiku kuwa nyumba yangu inaungua na imeteketea yote kwa moto,” Batuli aliiambia Clouds FM. 
Batuli nyumba
“Iliniuma sana vitu vilivyonusurika ni magari yangu tu mawili,” alisema kwa uchungu. Aliongeza kuwa majirani walihisi chanzo cha moto huo kinaweza kuwa ni umeme. Hata hivyo hakuna mtu aliyejerehiwa. Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na watoto wake na wafanyakazi wake wawili. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo