Ray C abadili msimamo kuhusu mwanaume wa kumuoa, asema wanaume wa mitandaoni hamna kitu

Ray C anaweza kuwa amezivunja roho za wanaume zaidi ya 500 waliojipanga mstari kujibu ofa yake aliyoitangaza kwenye Instagram kuwa anatafuta mume.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bongo5 Ray C amesema kuwa mume mwema hatafutwi kwenye mitandao bali huletwa na mwenyezi Mungu

“Huo ulikuwa utani tu,” amesema Ray C. “Nilikuwa nataka kuwafurahisha kidogo watu wangu wa Insta. Watu wengi sana, nimepata simu nyingi kweli kweli. Nimepokea zaidi ya simu 500 mpaka saa sita usiku. 

Kwahiyo nimeona mashabiki wangu bado wapo, wananipenda sana,” amesema. 

“Hapana sina mpango wa kuolewa. Mume mwema anatoka kwa Mungu, huwezi kusema unatangaza. 

Mume mwema anatoka kwa Mungu nikimpata mtasikia, sasa hivi sipo kwenye mahusiano, sina mtu yoyote.” 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo