Waziri
wa ujenzi Dr John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi na
kukamatwa kwa aliyekuwa mhandisi mshauri wa jengo la ghorofa moja la
ofisi ya mkuu wa wilaya ya Siha kwa kujengwa chini ya kiwango ili ajibu
tuhuma zinazomkabili na kutoa wiki mbili kwa uongozi wa wakala wa nyumba
(TBA) kukararabati jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Siha na mkuu wa
wilaya ya Moshi ambayo yameonekana kutofaa kwa matumizi ya binadamu
kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Waziri Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kutoridhishwa na hatua
zilizochukuliwa kushughulikia suala hilo baada ya kutembelea na kukagua
jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Siha ambalo halifai kwa matumizi ya
binadamu kutokana na kujengwa chini ya kiwango na kutoa maagizo kwa
uongozi wa wabunifu na wakadiriaji majenzi pamoja na msajili wa
wakandarasi.
Akitoa maelezo mbele ya waziri Magufuli afisa mtendaji mkuu wa
wakala wa nyumba Elius Mwakalinga amemwambia waziri kuwa usanifu michoro
ya jengo hilo ilikuwa sahihi lakini tatizo ni la mkandrasi ambe
hakufuata vigezo vya ujenzi wa jengo hilo.
Katika tukio jingine akizungumza na wananchi wa Ngarenairobi waziri
Magufuli amewahakikishia wananchi hao kuwa barabara ya kwa sadala
kupitia sanya juu hadi Ngarenairobi itajengwa kwa kiwango cha lami baada
ya waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Aggrey Mwanry kumwambia waziri
magufuli adha wananchi ho wnayoipata ikiwa ni pamoja na kushindwa
kusafirisha mazao yao pamoja kupanda kwa gharama za usafirishaji
hususani nyakati za mvua.
Waziri Magufuli amehitimisha ziara yake mkoani Kilimanjaro ambapo
akiwa njiani kurejea Dar es Salaam anatarajiwa pia kukagua ujenzi wa
daraja la Kariakoo katika bonde la ruvu katika barabara ya Bagamoyo
msata mkoani Pwani.