SIKU chache baada ya picha za mtoto mchanga kusambazwa katika
mitandao ya kijamii na kudai kuwa ni za mtoto wa mwimbaji wa nyimbo za
Injili nchini, Flora Mbasha kuwa amezaa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hatimaye wawili hao wamefunguka.
Hatua hiyo imekuja miezi saba tangu wawili hao walipoingia katika
mgogoro wa ndoa yao hali iliyosababisha mume wa Flora, Emmanuel Mbasha
kufikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji.
Mchungaji Gwajima, alisema taarifa hizo ni za uzushi na huenda zinasambazwa na mume wa Flora.
Mchungaji Gwajima alikwenda mbali na kusema pamoja na uzushi huo
unaosambazwa dhidi yake kwa kuhusishwa katika uhusiano na Flora
anamwachia Mungu kila kitu.
“Hahaha… si unajua hiyo issue
(suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu… wakati mwingine mimi huwa
sijibu ujinga,” alisema Gwajima huku akicheka.
“Awali niliwaza kuwashitaki
(alipoanza kuhusishwa kwamba ana uhusiano na Flora) wanaoeneza uzushi
huo lakini nikaona ‘It doesn’t hold water’ (haina mashiko), najua
shutuma hizo zinatoka wapi:-Gwajima.
“Mimi sikujua kama alikuwa
mjamzito, hata taarifa kwamba amejifungua ndiyo nazisikia kwako. Hapa
nimetoka ‘airport’, sikuwepo Dar es Salaam.
Flora akizungumza kwa njia ya simu alisema “Siko
tayari kuzungumza lolote kuhusu Mbasha kwa sasa. Yeye anajeuri ya pesa
ndo maana anafanya haya yote lakini mimi ninasimama na Mungu wangu na
ninajua Mungu atanipigania:-Flora.