Spika
wa Bunge Anna Makinda jioni Ya jana amelazimika kuahirisha tena kikao
cha
Bunge hadi kesho asubuhi kwa madai kuwa serikali bado inajipanga
kutoa majibu sahihi kutokana na tukio la kupigwa mabomu
Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Kuahirishwa kwa bunge kumetokana na vurugu zilizotokea jana asubuhi bungeni baada ya
kutolewa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa Ibrahimu Lipumba jana akiwa kwenye maandamano .