Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola,
marehemu Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika
Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana
Oktoba 13, 2014.
Spika
wa Bunge la Jamhuri, Mhe. Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho mbele
ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, wakati
wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake, Nyampande Wilaya ya
Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha
Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William
Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini kwake,
Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka Shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama
cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt.
William Shija, wakati wa shughuli za maziko yaliyofanyika Kijijini
kwake, Nyampande Wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza, jana Oktoba 13,
2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini katika Kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu
wa Chama cha Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu
Dkt. William Shija, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika Kijijini
kwa marehemu, Nyampande Wialaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza jana, Oktoba
13, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bialal, akiwafariji wanafamilia wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha
Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William
Shija, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika Kijiji ch Nyampande
Wilaya ya Sengerema, Mkoa wa Mwanza jana, Oktoba 13, 2014.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika
nyumbani kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Madola, marehemu Dkt. William Shija, Kijiji cha
Nyampande Wilaya ya Sengerema, jana Oktoba 13, 2014. Picha na OMR
Makamu wa rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ambaye aliwahi kufanya
kazi pamoja na Dk. William Shija kama katibu mkuu wa wizara ya Sayansi,
Teknolojia na elimu ya juu kwa miaka 10 amesema kuwa marehemu Dk.
William Shija alikuwa mchapakazi hodari, mwenye bidii, mwadilifu na
aliyependa watu, hivyo kifo chake ni pigo kubwa siyo tu kwa watanzania
bali katika jumuiya ya kimataifa ambako amehudumu kama mtu wa kwanza
mweusi kuwa katibu mkuu wa mabunge ya jumuiya ya madola tangu kuanzishwa
kwa jumuiya hiyo mwaka 1911.
Kwa upande wake spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mh. Anne Makinda amesema upinzani sio uadui, na kuwataka wanasiasa kuiga
mfano wa maisha ya Dk. William Shija ya uadilifu na kutojilimbikizia
mali huku mwakilishi wa bunge la Kenya Seneta Moses Watangula akisema
kwamba umoja wa mabunge ya jumuiya ya madola umeondokewa na mtu shujaa
ambaye alisimama imara kupinga kila aina ya ubaguzi uliokuwa ukifanywa
na wazungu dhidi ya waafrika.
Mtoto wa marehemu Dk. Shija, Anna- Claire Shija amesema familia
hiyo daima itaendelea kumuenzi marehemu baba yao kwa matendo mema,
ambapo Padri Revocatus Makonge wa parokia ya Nyampande akihubiri katika
ibada ya misa yamazishi iliyoongozwa na askofu wa kanisa katoliki jimbo
la Bunda ambaye pia ni msimamizi wa kitume wa jimbo la Geita mhashamu
Renatus Nkwande walikuwa na haya ya kusema marehemu Dk. William Shija
ambaye alizaliwa mwaka 1947 wilayani Sengerema ameacha mjane na watoto
watano.