Jukwaa
la Katiba Tanzania (JUKATA), Deusi Kibamba (katikati) akiongea mbele ya
mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Akionyesha tofauti ya Katiba mpya na ile ya zamani. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Siku
chache baada ya Mjumbe wa bunge Maalum la katiba ambaye pia ni Makamu
Mwenyekiti kupitia chama cha NCCR Mageuzi - Zanzibar, Haji Ambar Hamis
kutoa tuhuma za kupigishwa kura ya kupitisha Katiba inayopendekezwa bila
ridhaa yake.
Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) nalo limetoa tuhuma kwa kitendo cha
udanganyifu kwa upande wa Zanzibar ambapo Mheshimiwa Zakia Megji
amewekwa kama mjumbe kutokea Zanzibar na wakati yupo upande wa Tanzania
bara.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa JUKATA, bwana Deus Kibamba jijini
Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wahabari.
Aidha Kibamba amesema kwamba katiba inayopendekezwa imeshindwa kukata
kiu ya Watanzania walio wengi kuhusu namna ya kutatua tatizo la kushuka
kwa maadili ya viongozi na watumishi wa umma katika Taifa.