HAMISA MOBETO AMUONESHA MCHUMBA WAKE, NI DJ MAJAY WA EFM

Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto ameamua kumwanika mwandani wake baada ya kumuweka kwenye mitandao ya kijamii  huku akimmwagia sifa kemkem.
Mwanadafada ambaye ni mwanamitindo Bongo, Hamisa Mabeto akila ujana na mpenzi wake.

Akipiga stori na mwandishi baada ya kuvutiwa waya, Hamisa alisema mwanaume huyo ambaye ni miongoni mwa wakurugenzi wa redio EFM aitwaye Dj Majay ni mtu ambaye anampenda sana na wana malengo ya kuoana muda wowote kuanzia sasa na jina lake ataliweka hadharani soon!

“Ni kweli ni mpenzi wangu ambaye tunapendana sana na muda wowote kuanzia sasa tutafunga pingu za maisha kama mipango yetu ikikaa vizuri,” alisema Hamisa.

Aliendelea kusema kuwa wana miezi sita mpaka sasa na amekuwa mtu ambaye anajua nini thamani ya mapenzi kwani muda wowote akimuhitaji anakuwa karibu yake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo