WATU 93 WAKAMATWA KWA KUVAMIA SHULE JIJINI MBEYA



Jeshi la polisi Jijini Mbeya linawashikilia wananchi wa kijiji cha Lupembe Wilayani Kyela wapatao 93 kwa kuvamia shule ya sekondari Mwingo wakiwa na silaha mbalimbali za jadi.

Wananchi hao wamefanya uvamizi huo kwa kile kinachoelezwa kuwa walikuwa wakiwataka walimu na wanafunzi wa shule hiyo waondoke katika eneo la shule wanalodai kuwa ni mali ya kijiji.
 
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Kamishana msaidizi wa polisi Barakael Masaki amesema Chanzo cha fujo hizo ni Mgogoro wa mpaka wa shule hiyo na eneo la kijiji.
 
Kamishana Masaki ametoa wito kwa jamii kufuata sheria katika kudai haki zao kwa njia ya amani na utulivu ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo