BAADA YA KUNYAKUA TUZO YA AFRIMMA, HII NDIO TAREHE YA LADY JAY DEE KUWASILI HAPA NCHINI AKITOKEA MAREKANI



Anaconda, Lady Jay Dee ambaye ameshinda tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji bora wa kike Afrika Mashariki atatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, August 3 mwaka huu akitokea Marekani.

Akiongea na mwandishi, meneja wa Lady Jay Dee, Captain Gardener G. Habash amesema kuwa mwimbaji huyo anatarajia kuondoka Houston, Marekani August 1 na kuingia Dar es Salaam August 3.
 
Amesema Lady Jay Dee yuko Marekani alikuwa ameenda kwa ajili ya likizo au mapumziko.
 
Tuzo hiyo ya AFRIMMA imekuwa tuzo ya 30 kwa muimbaji huyo, idadi hiyo ilifahamika rasmi baada ya kuandika ujumbe wa shukurani kwa mashabiki wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo