Sheikh Mohammed Idris enzi za uhai wake.
Sheikh Mohammed Idris, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na
Wahubiri nchini Kenya, ameuawa karibu na msikiti ulio karibu na nyumba
yake na watu wasiojulikana leo asubuhi huko Mombasa.
Duru zinasema kuwa alikuwa amepokea vitisho kutoka kwa vijana wenye
itikadi kali za kidini na tayari alikuwa ameelezea hofu juu ya maisha
yake.
Wengine waliuawa kwa madai ya kuwa na uhusiano wa karibu na kundi la
wanamgambo la al-Shabaab huku wafuasi wao wakiilaumu serikali kwa mauaji
yao, madai ambayo serikali imakanusha.
Marahemu Idris alikuwa ameitaka serikali kukabiliana na baadhi ya
watu wenye itikadi kali za kidini ndani ya msikiti hali ambayo
ilisababisha baadhi ya waumini kumuita msaliti.
