
Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko
kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya
kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku
wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini
kuwa ni watu wanaohitaji msaada.
Cha
kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika
kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye
kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30.
Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari
wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu
hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana.
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa
matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine
aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani,
na kwenye paja la mguu wa kulia.
Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni.
Kwa
mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME,
anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo
Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina.
Kazi
ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na staili hii ya
ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni
kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali
mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana
na wahusika wa tukio hili. AMEN