KIJANA AUAWA NA WANANCHI KWA TUHUMA ZA WIZI WA TV NA SOLAR WILAYANI KAHAMA



Kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 28-30 ambaye hajafahamika jina lake wala makazi ameuawa na wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira kwa tuhuma za wizi katika mtaa wa Muhongolo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa tatu asubuhi baada ya kudaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa ndani kwenye nyumba ya jirani ambayo hata hivyo haijatajwa, ambapo alijifungia ndani kabla ya wananchi kuvunja mlango na kumtoa.

Imedaiwa kuwa Kijana huyo amewawa akituhumiwa kuhusika na wizi wa TV na Solar katika maeneo ya mtaa huo, na kwamba amekuwa akifanya uhalifu mara kwa mara lakini amekuwa akiendelea kuonekana mtaani hata baada ya kukamatwa na polisi. 
 
Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo