Brazil imeponea kung'olewa kutoka mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini humo.
Hii ni baada ya mechi ya kwanza ya mkondo wa
muondoano kati yake na Chile kumalizika kwa mikwaju ya Penalti baada ya
timu hizo mbili kwenda sare ya bao moja baada ya kipindi kizima cha
mechi.
Na pia baada ya kucheza muda wa ziada.
Wakati wa mikwaju ya Penalti, Brazil iliingiza tatu huku Chile ikiingiza mbili.
Wakati wa mechi , Brazil iliingiza bao la kwanza
la mechi ndani ya kipindi cha kwanza, lakini Chile ilileta jibu kabla
ya kipindi cha kwanza cha mechi kukamilika.
Brazil ilikuwa na kibarua kigumu na shinikizo
tele kutoka kwa mashabiki wa Brazil ambao walijaa uwanjani na pia kwa
kuwa Brazil ni mwenyeji wa michuano hiyo ,matarajio ya wengi nchini
Brazil ni kuwa wanatafanya vyema katika mashindano hayo.
Kufungwa
kubaya,wachezaji wa Chile wakitoka uwanjani kichwa chini baada ya
kutolewa kwa penalti na Brazili katika michuano ya kombe la dunia
inayoendelea huko nchini Brazili.
Shujaa wa
Brazili mlinda mlango Julio Cesar aliokoa mikwaju miwili ya penalti
dhidi ya Chile na kuisaidia timu yao kutinga hatua ya robo fainali.
Wachezaji wa Brazili wakimpongeza mlinda mlango wao Julio cezar baada ya kuokoa mkwaju wa kwanza wa penalti kutoka kwa Chile.
Beki wa Brazili David Luiz akishangilia goli lake la penalti dhidi ya Chile.
Baada ya
dakika 90 za maumivu sasa vijana wanajipanga kwa dakika 120 ili kutafuta
mshindi wa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la dunia 2014.
Mpambano
ulikua siio mchezo ndani ya dakika 120, huyo hapo juu ni msukuma ndinga
wa Chile akigangwa baada ya kupata mshike mshike uwanjani.
Mchezaji wa
Chile akipiga penalti ambayo iligonga mwamba na kurudi uwanjani na kuipa
tiketi Brazili kutinga robo fainali ya kombe la dunia nchini Brazili
baada ya kazi nzuri waliyoifanya dakiak 120 na kutoka sare ya 1-1.
Umoja ni nguvu,baada ya dakika 120 sasa wabrazili wanakumbatiana kutiana moyo kuelekea kwenye mikwaju ya Penalti.