WAZAZI WAFANYA SHEREHE KUFUATIA WATOTO WAO KUFELI MITIHANI RUVUMA



Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu amesema kuwa Serikali ya Mkoa huo imewafikisha mahakamani wazazi 100 kwa tuhuma za kufanya sherehe baada ya watoto wao kufeli mitihani.

Pamoja na wazazi/walezi hao kujitetea kuwa walikosa karo ya kuwapeleka watoto hao shule, imeelezwa pia kuwa mazingira duni ya kufundishia na kujifunza katika Wilaya ya Tunduru,  yameelezwa ni moja ya sababu inayowafanya wazazi kushawishi watoto wasisome kwa bidii wala kufaulu mitihani, ambapo mwanafunzi akifeli mtihani wa darasa la saba hufanyiwa sherehe.
 
Imeelezwa pia kuwa wanafunzi wanaosoma katika Shule za msingi Wilayani Tunduru mkoani humo huambiwa na wazazi wao kuwa wasijaze majibu yaliyo sahihi wanapofanya mitihani, bali wajaze ‘makorokocho’ ambapo kila anayefeli mtihani huo hufanyiwa sherehe na Wazazi wake.
 
Hali  hiyo  imeelezwa kuchangia kuifanya Wilaya hiyo kuwa ya mwisho Kimkoa na Kitaifa katika matokeo ya darasa la Saba mwaka jana.

 Hali ya Mkoa huo kielimu nayo hairidhishi kutokana na kuchangiwa kwa mwamko mdogo uliopo kwa wazazi na walezi.

>>>>>FIKRA PEVU


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo