Kundi
la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga ambalo liliwavuta mashabiki wengi
Tanzania kwa nyimbo zenye ujumbe wa maisha halisi ya Kitanzania mwaka
2001 walipotoa album ya Ukweli Mtupu, limepanga kurudi tena mwaka huu.
Kundi
hilo linaloundwa na Mkoloni na Dr. John, limeanzisha ukurasa mpya wa
Facebook ikiwa ni sehemu ya miradi ya ujio wao ili waweze kuwa karibu
zaidi na mashabiki wa sasa ambao wengi wako kwenye mitandao ya kijamii.
“BAADA
YA KUTOREKODI KWA PAMOJA KAMA KUNDI KWA MIAKA 8,SASA WAGOSI WA KAYA
TAYARI TUMESHAREKODI NYIMBO KADHAA AMBAPO WIKI HII TUNATARAJIA
KUTAMBULISHA KAZI TULIZOFANYA UKIZINGATIA UKIMYA WA MUDA MREFU ULIOKUWA
UMETAWALA KATIKA MUZIKI WETU WA HIP HOP........stay tuned!” Wagosi wa
Kaya wameandika kwenye ukurasa wao wa Facebook uliopokelewa na comments
nyingi za mashabiki wanaotamani kusikia tena kutoka kwao.
Huenda ‘Gahawa’ likawa ni jina la wimbo wao mpya kwa kuwa ndio jina liliwekwa mbele kwenye picha yao ya pamoja.
Post nyingine za Wagosi wa Kaya zinaonesha kuwa audio za nyimbo zao zitaambatana na video.
