MAHAKAMA YA WILAYA YA MAKETE YAMWACHIA HURU MWANAMKE ALIYEKUWA AKITUHUMIWA KUJERUHI

Mahakama ya wilaya ya Makete imemuachia huru Bi.Agness Tweve mkazi wa kijiji cha Iwawa kata ya Iwawa wilayani Makete Mkoani Njombe aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la kumjeruhi Donad Daud Sanga mkazi wa Iwawa Wilayani hapa.

Akitoa uamuzi wa kumuachia huru bila masharti Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Makete Mh.John Kapokolo amesema kuwa Mahakama imemuachia huru mtuhumiwa kutokana na ushahidi uliotolewa kutokuwa na vielelezo vya kuaminika mahakamani kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo.

Hata hivyo ushahidi uliotolewa haukuwa wa wazi na kubainisha namna gani mjeruhiwa ajeruhiwa na kuathirika kwa kiasi gani kwani inaonyesha mshitakiwa alipatwa na hali mbaya      

Wakati huo huo ndugu Manenge Sanga mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Ilevelo kata ya Lupalilo wilayani Makete amefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 65 mkazi wa kijiji cha Ilevelo.

Akisoma mashtaka hayo mwendesha mashtaka wa jeshi la Polisi Wilayani Makete Bw.Gozbet Komba amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 7 Julai 2013 saa mbili usiku katika kijiji cha Ilevelo ambapo alimvamia mshtaki akiwa nyumbani kwake na kumbaka  mama huyo ambaye pia ni Mjane.

Hata hivyo mshitakiwa amekana kuhusika na mashitaka, ikiwa mwendesha mashitaka wa polisi Bw.Komba ameiomba Mahakama kuwaleta mashahidi wa shitaka hilo katika tarehe iliyopangwa ambayo ni tarehe 20 Desemba mwaka huu.
 
Na Henrick Idawa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo