MWIGIZAJI wa kike wa filamu mwenye jina kubwa Bongo Wema Sepetu
‘Madam’ hivi karibuni alimpoteza baba yake mzazi aliyefariki katika
Hospitali ya TMJ kufuatia msiba huo Wema alifunguka kwa kudai kuwa baba
yake kilikuwa ni kiungo muhimu sana katika harakati zake za urembo na
sanaa kwa ujumla kwani baba yake alimuunga mkono katika kufanikisha
ndoto zake.
“Nimepoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu baba alikuwa
akinisupport katika sanaa kwani hata awali nilipotaka kuingia katika
mambo ya ulimbwende baba yangu aliniunga mkono, kulingana na nafasi yake
kwa mzazi mwingine isingekuwa rahisi kunikubalia kuingia katika
mashindano ya umiss,”anasema Wema.
Wema anasema hadi dakika za mwisho kabla ya baba yake kufariki
alikuwa akimwita Miss world, hata alipoingia katika sanaa ya uigizaji wa
filamu bado mzazi wake huyo alimuunga mkono jambo ambalo kwake lilikuwa
ni faraja na kujivua kuwa na mzazi anayetambua umuhimu wa kipaji cha
mwanaye.