WAZEE NA WATOTO MKOANI NJOMBE WANUFAIKA NA SHIRIKA LA TANWATT

Mzee Nicolaus Msigwa Ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi Cha Wazee Wanaopata Huduma Mbalimbali Kutoka Kampuni Ya TANWATT Kibena.
 
Na  Gabriel  Kilamlya Njombe.

Serikali Mkoani Njombe Imetakiwa Kutumia Fursa Zilizopo Katika Kuwasaidia Wazee Juu Ya  Utoaji wa Huduma za Afya Ili Kudumisha Sera ya Taifa ya Wazee Ya Huduma ya Afya Bure Kwa Wazee Wenye Umri Kuanzia Miaka 60 na Watoto Wenye Umri Chini ya Miaka Mitano.

Rai Hiyo Imetolewa na Mratibu wa Kitengo cha Kuratibu Ukimwi Katika Kampuni ya TANWATT Kibena Mjini Njombe Bi.Betty Liduke Wakati wa Semina ya Wazee Iliyofanyika Jana Katika Hospitali ya Tanwatt Iliyopo Kibena Mjini Hapa.

Bi.Liduke Amesema  Katika Kuwaenzi Wazee Ambao ni Hazina Ya Taifa Serikali Haina Budi Kutumia Mbinu Mbalimbali Ziweze Kuwasaidia Wazee Hao Ambao Wanahitaji Msaada Mkubwa Katika Maisha yao Hususani Katika Suala la Matibabu Bure.

Akielezea Hali ya Kundi la Wazee Hao Ambao Kampuni ya TANWATT Iliwakusanya Katika Maeneo Tofauti ya Mitaa ya Kibena na Kuwasaidia Kwa Misaada Mbalimbali Ikiwemo Huduma ya Afya ya Bure Kila Mwezi Bi.Liduke Amesema Kuwa
Kundi Hilo Lilianzishwa Mwaka 2012 Likiwa na Wazee 50 Ambao Kwa Sasa Wamebaki 48 Baada ya Wazee Wawili Kufariki Dunia.

Akizungumza Kwa Niaba ya Wazee Hao Mwenyekiti wa Kikundi Hicho Mzee Nicolaus Msigwa  Amewaomba Wadau Mbalimbali Kujitokeza Kuwasaidia Kutokana na Hali Ngumu ya Maisha Waliyonayo Kwani Serikali Bado Haijafanikiwa Kuwasaidia Licha Sera Kuwekwa Wazi.

Akizungumza na Wazee Hao Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Afisa Ardhi wa Mji wa Njombe Bwana Thadei  Kabonge Amepongoza Jitihada Kubwa Zinazofanywa na Kampuni ya Tanwatt Huku Akisema Suala la Wazee Atalifikisha Kwa Mkuu wa Mkoa Ili Liweze Kupatiwa Ufumbuzi Licha Ya Kuwa Serikali Bado Haija Fanikiwa Kutekeleza Sera Ya Wazee.

Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Wazee Hao Wamekuwa na Utaratibu wa Kukutana Kila Mwezi na Kampuni ya Tanwatt Huku Kampuni Hiyo Kwa Kushirikiana na Wadau Mbalimbali Wamekuwa Wakiwapa Misaada Mbalimbali Zikiwemo Nguo,Sabuni,Dawa za Meno Pamoja na Sukari Ili Kujikwamua na Umasikini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo