KWA HILI SERIKALI ITAZIDI KUPONGEZWA WILAYANI MAKETE

Kwa hivi sasa bila kuficha wala kuupindisha ukweli, serikali haikwepi pongezi kwa kuboresha barabara kutoka Njombe - Makete kwa kuwa awali hali ilikuwa mbaya

Kiufupi tangu niingie kwenye wilaya hii mwaka 2008 hali ya barabara ilikuwa mbaya kiasi kwamba kutoka Makete hadi Njombe ilikuwa zaidi ya masaa 12 hasa wakati wa masika

Kwa kawaida kutoka Makete hadi Njombe ni umbali wa kilomita 110, ukisafiri kwa basi ni takriban masaa 3 hadi 5 unakuwa umefika, kwa kipindi hicho ilikuwa ndoto kusafiri kwa masaa hayo tofauti na sasa unakwenda Njombe na kurudi

Miongoni mwa maeneo yaliyokuwa korofi kwa kipindi hicho cha mwaka 2008 ni Mago, Tandala, Usungilo na Mang'oto ambapo ilikuwa ni jambo la kawaida kwa abiria kushuka na kusukuma magari wanayosafiria na pia magari lazima yawe na chepe na kamba kwa ajili ya shughuli hiyo

Tujukumbushe tulipotoka kupitia picha hizi ambazo zilipigwa mwezi machi 2008 kwa kweli hali ilikuwa mbaya:-
Jionee mwenyewe hali ilivyokuwa.
 Abiria wakishirikiana kwa pamoja kulivuta basi lao lilipokwama meneo ya Usungilo
Kwa sasa eneo hili lililopigwa picha hizi limewekewa lami na hakuna usumbufu huu tena katika eneo hilo na barabara ya Njombe makete kwa ujumla inapitika misimu yote ya mwaka bila usumbufu kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma

Ama kweli jitihada za mbunge wa jimbo la Makete Dkt. Binilith Mahenge na wadau wengine walilivalia njuga suala hili hadi barabara hii ikawekewa lami katika maeneo yale korofi kama unavyoona hapo juu na kusababisha usafiri kuwa mrahisi kuliko ilivyokuwa kipindi cha nyuma

Imeandaliwa na Edwin Moshi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo