skip to main |
skip to sidebar
JUMUIYA YA WAISLAM WA MADHEHEBU YA SHIA, WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU MUHIMBILI
Jumuiya
ya Waislam wa madhehebu ya Shia ambao wanaadhimisha Siku ya Ashura
kukumbuka kifo cha mjukuu wa Mtume pamoja na jumuiya ya Patel Samaj za
jijini Dar es Salaam jana zimejitokeza kwa ajili ya kuchangia damu
kusaidia kukidhi mahitaji kwa wagonjwa katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa zoezi la utoaji damu, Afisa uhamasishaji Damu
Salama Bwana Lucas Michael amesema zoezi hilo ni mchango mkubwa kutoka
wanajumuiya hizo katika kukabiliana na upungufu wa damu kwenye Benki ya
Damu na kwamba katika zoezi hilo walitarajia kukusanya lita 300 hadi
400.
Bwana Michael amewahamasisha wananchi wengine wajitokezee
katika zoezi la utoaji damu kitaifa linalotarajiwa kuanza Jumatano
Novemba 13 nchini kote.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi