Baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuigiza filamu, mrembo na
mtangazaji, Jokate Mwegelo ameigiza kwenye filamu iitwayo ‘Mikono
Salama’ akiwa pamoja na Irene Uwoya na Single Mtambalike maarufu kama
Richie.
Kwenye filamu hiyo ya kampuni ya JB, Jerusalem Film Company na
iliyoongozwa na Adam Kwambiana na John Kalaghe, Jokate ameigiza kwa jina
la Ndekwa.
“Richie ameigiza kama rafiki yake na kaka yangu ambaye anatoka
vilevile na wifi yangu na baadaye ananitaka mimi na tunaishi pamoja
lakini vitu haviendi sawa,” Jokate ameiambia tovuti ya Bongo5.
“Wifi yangu atakuja na atakuwa anamtishia maisha sababu yuko na
mimi. So kidogo yupo kama half my boyfriend, half my protector but sio
mtu ninayempenda.”
Irene Uwoya ndiye aliyeigiza kama wifi yake na Jokate kwenye filamu hiyo
Jokate amesema wakati wa kushoot filamu hiyo alikuwa akijikuta
akichoka mno kwakuwa hajaagiza kwa kipindi kirefu na shughuli ilikuwa
ikichukua siku nzima na nusu.
“Naweza nikaondoka home saa moja, narudi saa 10 usiku kwahiyo
nilikuwa nachoka sana. Nilikuwa nafanya kazi sana, kwangu mimi kidogo
ilikuwa inanisumbua. Lakini watu katika kampuni ya JB walikuwa
wakiniattend vizuri, nikichoka wanasikiliza, nakula nini, maji whatever
kwahiyo at least walinipa wepesi katika kucheza character yangu.”
BONGO5.COM