![]() |
| Mtu aliyejifanya Ofisa Usalama wa Taifa (Katikati)akitolewa katika mkutano wa hadhara Mjini Ushirombo wilayani Bukombe, mkoani Geita. |
Jeshi la polisi mkoani Geita kwa kushirikiana na Maofisa Usalama wa Taifa, limemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alipenyeza katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete akijifanya mmoja wa walinda usalama.
Awali mtu huyo alianza kazi ya kulinda katika mji wa Uyovu Lunzewe ambako alijipanga katikati ya walinzi wa rais jirani
na Jukwaa huku akikagua baadhi ya wananchi na kuwapanga wengine wakati Rais akizindua ujenzi wa Barabara ya Uyovu hadi Bwanga inayojengwa kwa kiwango cha Lami.
Mtu huyo ametambulika kuwa ni Kwamani Juma (45) na alikamatwa juzi jioni mjini Ushirombo katika mkutano wa hadhara akiwa amejipanga sawia karibu na jukwaa kuu alilokuwa amekaa Rais Jakaya Kilwete.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Leonard Paul amesema mtu huyo amekamatwa, kamanda huyo hakupenda kutoa ufafanuzi zaidi.
"Ndiyo kama umeona kwenye mkutano kilichotokea ndiyo hicho, sina cha zaidi," amesema Kamanda Paul.
