MUME ADAIWA KUMUUA MKE NA KUKIMBIA KUSIKOJULIKANA

Mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Nyambiti wilayani Kwimba, ameuawa kikatili na mumewe na muuaji kutokomea kusikojulikana.

Paschal Joseph anadaiwa kumuua mkewe Grace Joseph (20) kwa kumkata na kitu chenye ncha kali sehemu za shingoni na kisogoni.
 
Tukio hilo la kinyama limetokea jana saa 11.00 alfajiri katika kitongoji cha Kibara, kijiji cha Nyambiti nyumbani kwao na marehemu.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana jioni, mzazi wa marehemu Bwana Joseph Bahebe alisema, chanzo cha mauaji hayo unatokana na wivu wa kimapenzi mgogoro ambao ulikuwa ni muda mrefu na kwamba marehemu ameacha mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
 
Alisema marehemu na mumewe walikuwa wakiishi kijiji cha Goloma tangu mwaka jana na mgogoro ulipoanza walirudi nyumbani kwake na kuwasuluhisha lakini jana alfajiri, alishtushwa na kelele  na alipoenda chumbani kwao alikuta marehemu anatokwa damu nyingi mwilini na alifariki akiwa njiani akipelekwa hospitali ya wilaya

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Seleman Mzee amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo jeshi la polisi wilayani Kwimba linamtafuta mtuhumiwa ili afikishwe mbele ya sheria..


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo