MENGI AACHA GUMZO BAADA YA KUMWAGA MAMILIONI SEKONDARI YA WAMA ILIYOKO RUFIJI

Katika hali iliyowashangaza wengi akiwamo Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA, Mzalendo na mmiliki wa makampuni ya IPP Bwana Reginald Mengi ameahidi kutoa Tshs Bilioni moja kwa kutoa mil 200 kila mwaka kwa miaka mitano ili kuipa support shule ya WAMA Nakayama iliyopo Rufiji.

Shule hiyo ambayo imefanya mahafari yake ya kwanza kwa kidato cha nne leo hutoa full scholarship kwa wasichana waliotoka katika mazingira magumu na hatarishi.


Akiongea kumshujuru Mengi,Rais Kikwete alisema anamfahamu Mengi na wameshrikiana kwa mambo mengi hata kabla hajawa Rais. Mengi pia aameelezea kukunwa na Mama Salma Kikwete na Taasisi ya WAMA kwa kuwajali mabinti masikini kwani naye amekulia katika umasiki na anaufahamu vilivyo.


Mimi si mshabiki wa Serikali hii lakini kwa hili la WAMA kuwasaidia mabinti wenye mazingira magumu mama huyu anastahili pongezi


.Kwa mara ya kwanza nimesikiliza hotuba ya shule ambayo haijatoa ombi kubwa kwa Rais na waziri wa elimu ya kwamba changamoto zilizopo shule imejipanga kukabiliana nazo.


Hivi ndivyo shule zote zilitakiwa kuwa...zimejitoshelesha ili kutoa fursa sawa kwa wote kwani imebainika baadhi ya wilaya zinafanya udanganyifu na kuwachomeka watoto wa wakubwa hivyo kuwanyima fursa mabinti masikini na mayatima.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo