TFF YATANGAZA KUSOGEZA MBELE HATUA YA KWANZA YA USAJILI

 
Shirikisho la soka nchini TFF limetangaza kusogeza mbele hatua ya kwanza ya usajili wa wachezaji kwa msimu wa mwaka 2013/2014 hadi August 05 badala ya August 03 kama ilivyokuwa ikionyesha katika kalenda ya matukio.

Katibu mkuu wa TFF Angetille Osiha amesema uamuzi wa kusogeza mbele umetokana na kuchelewa kwa santuri ya usajili wa msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Angetille Osiah amesema santuri hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili nchini mpaka majira ya mchana hii leo walikuwa wakiifanyia kazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo