Pichani juu ni Askari wakikagua mwili wa Marehemu Erasto Msuya,mara baada kupigwa rasasi kwa majibizano na wanaodaiwa kuwa ni Majambazi.
========== ======= ========
Habari
zilizotufikia Kutoka chumba chetu cha habari,zinaeleza kuwa
mmoja wa Wafanyabiashara wakubwa wa Madini jijini Arusha,aliyejulikana
kwa jina la Erasto Msuya na pia ni mmiliki wa SG HOTEL mkoani
humo,amepigwa risasi zaidi ya sita na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi
na kufa papo hapo,habari zinaeleza na kubainisha zaidi kuwa Marehemu
alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao
hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara.
Habari zaidi tuvute subra kidoogo,tutazidi kufahamishana kadiri ya taarifa zitakapokuwa zikiingia.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.