MWANAMKE ALIYEMMWAGIA MWENZAKE SUPU YA MOTO AFUNGWA MIAKA 5 JELA


MAHAKAMA moja mjini Naivasha imemhukumu mwanamke mwenye umri wa miaka 34, miaka mitano gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kummwagia mwanamke mwingine supu moto.
Maria Waruhi alifikishwa mbele ya hakimu mkazi wa Naivasha, Bi Selina Muchungi na kushtakiwa kwamba mnamo Mei 19, 2012 katika mtaa wa Kabati, mjini Naivasha, alimmwagia mchuzi moto Bi Mary Wanjiku na kumjeruhi vibaya.

Mahakama iliambiwa kwamba Bi Wanjiku alikuwa ameenda sokoni ambako alikuwa akiuza matunda. Alipofika kibandani mwake, mshtakiwa alimmwagia supu hiyo ya githeri.

Mashahidi aidha walisema kwamba kabla ya kisa hicho, wawili hao walikuwa wamegombana baada ya Bi Wanjiku kumuuliza Bi Waruhi kwa nini alikuwa amemwaga supu katika kibanda chake.

Akisaidiwa na wanawake wengine sokoni humo, Bi Wanjiku aliripoti kisa hicho kwa polisi ambao walimkamata mshtakiwa.

Bi Wanjiku alitibiwa katika Hospitali ya Naivasha na kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Akitangaza uamuzi huo, Bi  Muchungi alikikashifu kisa hicho ambacho alikitaja kama kosa linalohitaji adhabu kali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo