BASI LA AIR BUS LAPINDUKA MISEYU MOROGORO

 
ABIRIA 23 waliokuwa wakisafiri na
basi la Air Bus linalofanya safari
zake kati ya Tabora na Dar
wamejeruhiwa wanne kati yao
vibaya baada ya basi hilo
kupinduka eneo la Maseyu, mjini
Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa
zilizotangazwa na Radio One ni
kwamba basi hilo lilipinduka
kutokana na mwendo kasi wakati
likijaribu kuyapita malori na
kupoteza muelekeo kabla ya
kupinduka.

Taarifa hizo zinasema kuwa,
majeruhi wameumia vibaya
maeneo ya kichwani, kifuani na
miguuni na wamekimbizwa
hospitali ya Mkoa wa Morogoro,
huku
wanne akiwemo dereva wa
basi hilo wenyewe wakiwahishwa
jijini Dar es Salaam katika
hospitali ya Muhimbili kwa
matibabu zaidi.

Kati ya abiria hao waliojeruhiwa
13 wamelazwa hospitali hiyo ya
mkoa wa Morogoro, na kwamba
taarifa zaidi zinaendelea
kufuatiliwa ili kujua
kinachoendelea, ingawa mpaka
sasa hakuna kifo chochote
kilichoripotiwa .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo